• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

VIONGOZI na watendaji Ruvuma waaswa kusimamia ugawaji rasilimali za Taifa kwa kuzingatia vigezo vya kitakwimu

Imewekwa kuanzia tarehe: June 20th, 2023

MKUU  wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas  amewaasa  viongozi na watendaji  katika ngazi zote za kiutawala kusimamia vema maendeleo kwa kugawa rasilimali za taifa kwa kufuata vigezo vya kitakwimu na sio upendeleo.

Kanali Thomas ametoa rai hiyo wakati anafungua semina ya uwasilishaji,usambazaji na uhamasishaji matumizi ya matokeo ya sensa kwa viongozi na watendaji  kutoka wilaya zote za mkoa wa Ruvuma,iliyofanyika kwenye ukumbi wa Parokia ya Bombambili mjini Songea.

“Rasilimali za Taifa ni za wote hivyo  haitakiwi kumpendelea mtu,kundi fulani au eneo fulani,badala yake zinatakiwa kugawanywa kulingana na mahitaji ya watu katika maeneo yao wakiwemo watu wenye ulemavu,wazee,vijana na wajasirimali wadogo wadogo’’,alisema Kanali Thomas.

Amesisitiza matumizi mazuri na bora ya matokeo ya sensa katika kufanya maamuzi yenye kufuata vigezo vya kitakwimu badala ya matakwa binafsi ya baadhi ya watu.

Hata hivyo ameyataja matokeo ya sensa mkoani Ruvuma yanaonesha kuwa idadi ya watu imeongezeka kutoka watu 1,376,891 mwaka 2012 hadi kufikia watu milioni 1,848,794 mwaka 2022 ikiwa ni sawa na ongezeko la watu 471,903.

Amesema matokeo hayo yanadhihirisha kuwa kiwango cha ukuaji wa idadi ya watu kimeongezeka kutoka asilimia 2.1 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 2.9 mwaka 2022 ikiwa ni chini ya kiwango cha kasi ya ongezeko la idadi ya watu kitaifa ambacho ni asilimia 3.2 kwa mwaka 2022.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa,matokeo ya sensa mkoani Ruvuma yanaonesha kuwa  watu 471,903 wameongezeka katika kipindi cha miaka kumi kutoka mwaka 2012 hadi 2022.

Kutokana na matokeo hayo ya sensa,Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa viongozi na watendaji kuhakikisha kuwa mipango yote ya maendeleo ya muda mfupi,muda wa kati na muda mrefu  inawekwa kwa kuzingatia idadi ya watu,mahitaji yao na hali halisi ya mazingira.

Awali taarifa ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt.Albina Chuwa iliyosomwa kwa niaba yake na Meneja wa Takwimu Mkoa wa Ruvuma Mwantumu Athuman kwenye mkutano huo,imeeleza kuwa utekelezaji wa sensa ya watu na makazi umefanyika katika awamu tatu.

Amezitaja awamu hizo kuwa ni maandalizi,zoezi la kuhesabu watu na uchakataji, uchambuzi wa taarifa zilizokusanywa,uandishi wa ripoti za matokeo ya sensa na usambazaji na mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa.

Amesema hivi sasa idara ya takwimu inaendelea na awamu ya tatu ya semina na mafunzo ambayo ilianza mara tu baada ya kumalizika zoezi la kuhesabu watu ambapo ameitaja mikoa ambayo imeshapata mafunzo hayo ni Dodoma,Kigoma,Dar es salaam,Lindi,Mtwara,Pwani na Ruvuma.

Mada ambazo zimetolewa kwenye mafunzo hayo ni matumizi ya matokeo ya sensa na mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi na watendaji mkoa wa Ruvuma.

Mada nyingine ni matokeo ya sensa ya Mkoa wa Ruvuma kwa ramani,mwongozo wa kitaifa wa usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa ya mwaka 2022 na mfumo wa upatinaji wa matokeo ya sensa kidijitali.

Wakizungumza baada ya kupata mafunzo hayo,Mwakilishi wa Vyama vya Siasa mkoani Ruvuma Elias Nchimbi  na Mwakilishi wa Viongozi wa Dini Rajabu Songambele ambaye pia ni Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Ruvuma wameishukuru serikali kwa kuwashirikisha katika hatua zote za sensa ya watu na makazi hali ambayo imejenga hamasa kubwa ya matumizi ya takwimu katika jamii.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.