Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Komred Oddo Mwisho, amewataka viongozi wa chama hicho kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaondoa wenzao madarakani bila kufuata taratibu.
Akizungumza katika ziara yake kwenye kata za Wino na Gumbiro, amesisitiza kuwa mshikamano wa chama unategemea utii wa sheria na kanuni zilizowekwa.
Mwisho ameitaja Ilani ya CCM inaelekeza taratibu sahihi za kufanya maamuzi ndani ya chama, hivyo viongozi wanaokiuka sheria wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni.
Ameagiza wale waliowekwa pembeni bila kufuata utaratibu warejeshwe kwenye nafasi zao mara moja ili kudumisha haki na umoja ndani ya chama.
Pamoja na masuala ya uongozi, Mwenyekiti huyo amesikiliza changamoto za wananchi wa kata hizo, zikiwemo uhaba wa maji safi, umeme na miundombinu duni ya barabara.
Amewahakikishia wananchi kuwa serikali na chama vinaendelea kushughulikia matatizo hayo kwa kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi.
Baadhi ya wananchi, akiwemo Casto Joseph Mgaya na Albert Elnaus, wamempongeza Mwenyekiti huyo kwa kutembelea maeneo yao na kusikiliza changamoto zao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.