Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Komred Oddo Mwisho, amewataka viongozi wa chama hicho kuepuka migogoro na badala yake kuelekeza nguvu zao katika kuwahudumia wananchi.
Ametoa wito huo wakati wa ziara yake katika Tarafa ya Nakapanya, Wilaya ya Tunduru, ambapo amesisitiza mshikamano ndani ya chama ili kufanikisha maendeleo kwa kasi.
Ziara hiyo ilihusisha mazungumzo na wanachama wa CCM kutoka kata nane, ambapo aliwataka viongozi wa chama kuwaelimisha wanachama kuhusu umoja na ushirikiano kwa ajili ya ustawi wa chama na wananchi.
Amesisitiza kuwa mshikamano ndani ya chama ni muhimu katika kuhakikisha maendeleo yanafikiwa kwa ufanisi.
Katika hotuba yake, Oddo Mwisho amewataka viongozi wa chama kushirikiana kwa karibu na viongozi wa serikali za mitaa ili kuhakikisha huduma za msingi zinawafikia wananchi.
Pia amewakumbusha wenyeviti wa vijiji na mitaa kuwa na vikao vya mara kwa mara kwa mujibu wa taratibu, huku akisisitiza kuwa madiwani wana wajibu wa kusimamia mikutano hiyo.
Pamoja na kuhimiza mshikamano, Oddo Mwisho amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa katika kuboresha miundombinu, huduma za afya, maji, na umeme.
Ameeleza kuwa serikali inafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, akitolea mfano ujenzi wa madarasa, madawati, na vyoo safi katika shule za msingi, kama vile Shule ya Msingi Ligoma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.