Kamati ya Amani Mkoa wa Ruvuma kwa kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na Rais Magufuli wamewaasa wananchi kuwa watulivu.
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Amani cha viongozi wa Dini Mkoa wa RuvumaMwenyekiti Alhaji Shekhe Shabani Mbaya ametoa pole kwa Taifa la Tanzania na kwa mama Janeth Magufuli na familia pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Mzalendo namba moja ametutoka kipenzi cha watanzania tumepatwa na mshituko mkubwa,tuna majonzi makubwa,kama viongozi wa dini tunamasikitiko makubwa sana ya kuondokewa na Jemedari wa Vita“.
Katibu wa Balaza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) Mchungaji Elimu Mwenzegule amesema tutamkumbuka kwa mengi ambayo amefanya katika uhai wake katika kutetea wanyonge na kutopenda mafisadi nchini na wahujumu uchumi.
Mwanzegule amesema Rais Magufuli alipenda nchi ya Tanzania na alihakikisha inajengwa na watanzania wenyewe katika kipindi chote alicholichokuwa madarakani alifanya kazi na watanzania hakupenda kutoka nje na alisema ni Rais wa watanzania na aliwatumikia kwa moyo.
“Tumepoteza kiongozi Jemedali na hodari Tunamuombea makamu wa Rais Mungu ampe uvumili katika kusimamia Maombolezo haya na kumpumzisha Mpendwa wetu, amevipiga vita vilivyo vizuri mwendo ameumaliza,Imani ameilinda Rais Magufuli katika nchi yetu na mwendo ameumaliza”.
Amesema anawatakia viongozi waendelee kuwa na mshikamano ili kuendeleza kazi nzuri alizoacha Rais,watanzania tuendelee kuwa pamoja tushikamane kwa utulivu katika wakati huu mgumu ambao tunapitia kwa tukio hili ambalo hatukulitalajia tushikamane,tutiane moyo.
Naye Makamu mwenyekiti wa Amani Mkoa wa Ruvuma Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Ruvuma Amoal Mwenda kwa upekee wake na kadri alivyozoeleka kwa kazi nzuri Mungu alimpa vipawa vyake katika utendaji kazi na kutokuwa na ubaguzi kwa watu wote.
Amesema viongozi wa Dini Mkoa wa Ruvuma tunaungana pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuwaomba wananchi wote kuwa watulivu huku tukishikamana na kuomboleza kwa umoja wetu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Machi 19,2021.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.