Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Dini Wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuzuia unyanyasaji wa kijinsia katika Mazingira yanayowazunguka.
Wito huo umetolewa katika semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, ambapo viongozi hao walikutana kujadili ustawi wa jamii kupitia mshikamano wa madhehebu ya dini.
Mada kuu iliyowasilishwa katika semina hiyo ilihusu "Namna Bora ya Kuzuia Unyanyasaji wa Kijinsia katika Mazingira Yanayomzunguka Mwanadamu."
Akizungumza wakati wa semina hiyo, Meneja wa Mradi wa Kuimarisha Mshikamano Miongoni mwa Madhehebu Mbalimbali ya Dini, Ndg. Erick Gallawa, amesisitiza jukumu la viongozi wa dini katika kuzuia unyanyasaji wa kijinsia kutokana na nafasi yao kubwa ya kuaminika katika jamii.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.