• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

VIONGOZI wa dini ,wazee Ruvuma washiriki maombi ya kuliombea Taifa kuelekea UchaguzI Mkuu

Imewekwa kuanzia tarehe: September 9th, 2020


MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewaongoza viongozi wa dini na wazee maarufu katika Mkoa wa Ruvuma katika maombi maalum ya kuombea Taifa kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Maombi hayo yamefanyika katika viwanja vya Ikulu Ndogo mjini Songea ambapo baada ya maombi wazee na viongozi wa dini  washiriki kula chakula cha jioni na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Akizungumza kabla ya maombi hayo Mndeme amewashukuru viongozi wa dini na wazee maarufu kwa kumuunga mkono Rais Dkt.John Magufuli katika kipindi cha miaka mitano iliyopita  ambapo amewashauri kuendelea kumuunga mkono ili maendeleo aliyoyaanzisha  aweze kuyamalizia katika kipindi cha miaka mitano iliyobaki.

Amesema Rais Magufuli katika kipindi cha miaka mitano amefanikiwa kuwaunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja ambapo Rais Magufuli akiwa kanisani alianzisha michango ya ujenzi wa msikiti jambo ambalo amesema  halijawahi kutokea katika historia ya Tanzania.

“Magufuli ni Rais ambaye amedhamiria kutuunganisha watanzania kwa hiyo tuna kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono,ili kasi hii ya maendeleo aliyoianzisha kwa wananchi aweze kuikamilisha’’,alisema Mndeme.

Mndeme amewaasa wazee na viongozi wa dini kuendelea kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwa kila jambo na kuendelea kumuombea Rais Magufuli afya njema na maisha marefu sanjari na kufundisha mafundisho mema kwa vizazi vyote vitambue kazi njema inayofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Amesema serikali ya Rais Magufuli inatarajia kutekeleza mradi wa ujenzi wa treni ya kisasa kutoka Mtwara hadi Mbambabay mkoani Ruvuma na kwamba watalaam wanafanya upembezi kwa ajili ya maandalizi ya mradi huo.

“Sisi wanaruvuma tutanufaika sana na miumbombinu hii ,unaweza kuamua kusafiri kwa gari,treni,meli  na ndege ,nawaambia haya kwa sababu mimi nimeshiriki na nimeona taarifa ya awali ya ujenzi wa reli ya Mtwara hadi Mbambabay’’,alisema.

Kwa upande  Mwakilishi wa viongozi wa dini Askofu Alimosa Mwasangapole wa Kanisa la TAG Songea  amesema viongozi wa dini wanaridhishwa na kazi ambayo anaifanya Rais Magufuli kutambua mchango wa dini katika maendeleo ya Taifa.

“Nimekuwepo tangu wakati wa uhuru,nimeona marais wote lakini huyu mtu ni wa pekee,kwa namna Rais Magufuli anavyowajengea watanzania imani kuhusu Mungu,huyu angepewa tu udaktari wa dini’’,alisema Askofu Mwasangapole.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Manispaa ya Songea Exavery Nyoni akizungumza kwa niaba ya wazee wa Mkoa wa Ruvuma amesema isingekuwa Ilani ya CCM kupitisha mgombea Urais kufanya kazi kwa miaka kumi wangependa Rais Magufuli afanyekazi ya Urais katika maisha yake yote.

“Huyu nasema ni mtoto wa Nyerere kwa sababu yale yote ambayo Nyerere aliyaotea huyu ndiyo anayafanya,ingekuwa sio Ilani ya CCM tungesema aendelee tu mpaka Mungu atakapotaka,kwa kweli Mkoa wetu wa Ruvuma hadi sasa tumepiga hatua kubwa katika maendeleo’’,alisisitiza Nyoni.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Ikulu Ndogo Songea

Septemba 8,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.