Picha ya kwanza juu ni kisiwa cha Lundo
Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imejaliwa kuwa na vivutio adimu vya utalii vikiwemo visiwa vitatu vya ziwa Nyasa vinavyoipamba wilaya hiyo kiutalii.
Visiwa hivyo ni Pamoja na kisiwa cha Mbambabay,Lundo na Puulu, ,ambavyo vimekuwa na sifa na historia nyingi ambazo zikitangazwa vizuri zitachangia kukuza utalii kwa kuvutia watalii wa ndani na nje.
Visiwa hivi kila kimoja kimekuwa na sifa ya pekee; kisiwa cha Mbambabay kina sifa ya kuwa na mapango ambayo wavuvi hujihifadhi wakati wa dhoruba kali,samaki wa mapambo pia wanapatikana katika kisiwa hicho.
Kisiwa cha Lundo kina historia ya kuishi wagonjwa wa ukoma waliotengwa na jamii na makaburi ya wagonjwa hao ambao walizikwa kwenye tope au kwa kugandikwa tope kwa imani kwamba wakifanya hivyo wangetokomeza ugonjwa huo.
Kisiwa kingine kinaitwa Puulu ambacho kipo Kata ya Liuli kimebarikiwa kuwa vivutio mbalimbali ikiwa na mazalia ya Samaki wa aina mbalimbali wakiwemo Samaki wa mapambo na makazi ya ndege maarufu duniani anayeitwa ngwazi mwenye uwezo wa kuvua Samaki.
Kisiwa cha Mbambabay
kivutio kingine maarufu ni uwepo wa jiwe la Pomonda lina pango kubwa ambalo linaweza kuhifadhi watu zaidi ya 100.Jiwe hilo wakati huo lilitumika kujificha wakati wa vita na wavuvi kujihifadhi dhoruba inapozidi,jiwe hili pia ni eneo zuri ambalo hutumiwa na waogeleaji kwa ajili ya kujirusha wakati wa mchezo wa kuogelea.
Kisiwa cha Puulu
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.