Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dkt, Benson Ndiege ameviambia vya Ushirika Wilaya ya Tunduru kubuni vyanzo vingine vya mapato
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kutembelea maghara pamoja na kushiriki hafla ya uzinduzi wa Ghala la Chama cha Namatili (AMCOS ltd) katika tarafa ya Nakapanya wilayani Tunduru mkoani Ruvuma
Ndiege amevitaka vyama ya ushirika kuwa na mipango ya kiuwekezaji pia kusubutu kushirikiana na taasisi nyingine kwa lengo la kuongeza vyanzo vingine vya mapato kwa kikundi na wanachama kwani itasaidia kukuza uchumi wao na wataona matunda
“Vyama vingine tuige huu ndio ushirika tuliokuwa nao kwanini leo tunashindwa hata kujenga ghala vyama vya ushirika vimekuwa vinaleta umasikini badala ya kuleta utajiri wito wangu mlitunze ghala hili na ongezeni miradi mingine sisi kama viongozi tutawasaidia” amesema Ndiege.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe, Julius Sunday Mtatilo amevitaka vyama vingine vya ushirika wilayani umo vione na viige mfano huu kutoka chama Namatili (AMCOS ltd) kwani chama hicho ndio kinafanya vizuri ngazi ya kitaifa hadi Mkoa
Amesema Huu ni uwekazaji na msihishie kwenye magari tu kama mnao uwezo mshirikishane na Mabanki ili muweze kuongeza vyanzo vingine vya mapato pia nisisitize kwenu mshirikiane na viongozi wenu ili waweze kutekeleza majikumu yao
“Niwapongeze chama Namatili (AMCOS ltd) kwa kuweza kufanya uwekezaji huu pia msichoke kuwasukuma viongozi wenu kwani itasaidia kufikia malengo pia mnapopata viongozi kama hawa mshirikiane nao”amesema Mtatilo.
Taarifa iliyosoma na makamu mwenyekiti Bi, Hawa Macheba wa Namatili (AMCOS ltd) inaeleza ujenzi wa Ghala hilo umegharimu shilingi Milioni sitini na tisa ambapo fedha hizo za ujenzi zimatokana na mapato ya chama hicho
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.