Mkuu wa Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma Kapenjama Ndile, amepongeza juhudi za wabunge Jenista Mhagama na Msongozi katika kusukuma mbele maendeleo ya wananchi.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Siku ya Wanawake Duniani katika viwanja vya Soko Kuu, Manispaa ya Songea, alisema wabunge hao wameonesha kujali wananchi kupitia mikakati mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.
Ndile alieleza kuwa Mbunge Msongozi ni mtu wa kujali wananchi, kwani kila anaporudi kutoka safari, hupitia ofisi za Mkuu wa Mkoa na baadaye ofisini kwake kuulizia changamoto zilizopo.
Aliongeza kuwa Mbunge huyo pia huchukua hatua haraka pale anapopokea taarifa za matatizo kutoka kwa wananchi wake.
Aidha, alimtaja Mbunge Jenista Mhagama kuwa ni kiongozi mwenye moyo wa kusaidia, kwani anapopokea taarifa za maafa au matatizo ya wananchi, huwa hawezi kuzihifadhi peke yake bali huzifikisha kwa wahusika ili kutafutiwa suluhisho.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema utendaji huo ni mfano wa uwajibikaji mzuri unaopaswa kuigwa na viongozi wengine.
Ndile alibainisha kuwa wabunge wanaofanya kazi kwa ukaribu na wananchi na kushirikiana na viongozi wa serikali mara nyingi huleta mabadiliko chanya katika maeneo yao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.