Wawekezaji wa Kampuni ya Xiwang kutoka nchini China wamepewa shamba lenye Hekari 10,000 lililopo Kijiji cha Ngadinda Kata ya Gumbiro Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma kwaajili uwekezaji wa kilimo cha mazao ya mifugo.
Mbunge wa Jimbo la Madaba Mheshimiwa Joseph Mhagama akizungumza kwenye eneo hilo amesema shamba hilo la Serikali lilikuwa na hekari 15,000 ambapo hekari 5000 wamepewa wananchi kwaajili ya kilimo.
“Wananchi mmepewa hekari 5000 na eneo lililobaki tunampa mwekezaji naomba tutoe ushirikiano kwa mwekezaji”,alisema Mhagama.
Meneja wa Kampuni ya XIWANG Savio Chanahi amesema wamejipanga kuzalishaji mahindi ya njano,soya na ufuta na watakuwa wanabadilisha mazao kwa kurutubisha ardhi ili kulinda mazingira.
Amesema Wizara itakapowakabidhi rasmi Shamba hilo ndani ya miezi miwili wataanza kupeleka vifaa kwa ajili ya kuanza kazi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.