Kikao Cha wadau katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma kimeazimia kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani Wilayani humo kutokana na mfumo huo kuonesha mafanikio makubwa kwa wakulima.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi wa vyama vya msingi 47 katika Wilaya ya Namtumbo , viongozi wa vikundi vya wakulima ,wanunuzi wa mazao ,viongozi wa wafanyabiashara ,kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Namtumbo ,wakuu wa idara , Taasisi za kibenki Pamoja na wamiliki wa maghala.
Akitoa taarifa ya uendeshaji mfumo wa stakabadhi ghalani Kwa msimu uliopita wa mwaka 2022/2023 Afisa Kilimo,Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Paul Ambokile amesema mauzo kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani umewanufaisha wakulima Kwa kiasi kikubwa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Msingi Namtumbo Asedi Kaporo amesema kuwa mfumo wa stakabadhi ni mzuri kwa kuwa wakulima wanauza mazao yao kwa bei kubwa tofauti na soko holela ambalo limekuwa linawanyonya wakulima.
Diwani wa Kata ya Mkongo Mheshimiwa Daniel Nyambo amesema mfumo wa stakabadhi ghalani unawanufaisha wakulima ambapo ametoa rai kwa wadau hao kuwadhibiti wafanyabiashara ambao hukopesha wakulima fedha ndogo na hulipwa ufuta mwingi na wao kuuza katika mfumo wa stakabadhi ya ghala na kujipatia pesa nyingi.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya amesema mfumo wa stakabadhi ghalani umewawezesha wakulima wa Wilaya ya Namtumbo kupata bei nzuri Kwa mazao ya ufuta,mbaazi na soya Pamoja na kuwa na uhakika wa soko.
Amewaagiza viongozi wa vyama vya msingi kuhakikisha wanasimamia mfumo Kwa uadilifu mkubwa na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kusimamia haki na maslahi ya wakulima .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Philemon Magesa amewataka wadau kushirikiana katika kuhakikisha mfumo wa stakabadhi ghalani una wanufaisha wananchi wa Namtumbo.
Magesa amedai kuwepo Kwa wafanyabiashara wanaonunua ufuta Kwa wakulima na wafanyabiashara wanaokopesha fedha Kwa wakulima Kwa fedha ndogo na wakati wa masoko Kwa mfumo wa stakabadhi ghalani unapoanza wafanyabiashara hao hupeleka ufuta na kulipwa fedha nyingi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.