MKUU wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile amewataka Waendesha Bodaboda na Bajaji kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali.
Ndile amesema hayo kwenye kikao maalum kilichowakutanisha madereva wa pikipiki miguu miwili (bodaboda) na pikipiki miguu mitatu (bajaji) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mkuu wa Wilaya Songea amewashauri madereva hao kuunda umoja wao ili kuwezesha kuwa na Sauti moja wanapokuwa changamoto mbalimbali na kuzifikisha kwa viongozi ili kutafutiwa ufumbuzi.
“Lengo la la kikao hiki ni kusikiliza kero zenu, mnapokuwa na uongozi imara mtaweza kupeleka changamoto zenu kwenye Mamlaka husika kwa kufuata utaratibu unaokubalika ambao pia utawezesha kupata fursa mbalimbali ikiwemo kupata mikopo, kupata mafunzo ya udereva kupitia VETA na kujenga mahusiano bora baina yao na Serikal”.alisisitiza Ndile.
Amewataka madereva hao kufuata sheria bila Shuruti ikiwemo kulipa leseni ya Udereva na Leseni ya Chombo chenyewe huku akitoa rai ya kuweka utaratibu wa kukutana mara kwa mara na madereva hao ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Kwa Upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Songea ASP Muya Zuberi Maunganya amewataka Waendesha Bajaji na Bodaboda kuzingatia Maegesho rasmi yaliyoruhusiwa na Mamlaka husika.
Nao Waendesha Bodaboda na Bajaji wameishukuru Serikali kwa kuitisha kikao hicho ambacho kimekuwa ni sehemu ya kutoa kero zao na kusikilizwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.