Tume ya Ushindani (FCC) Nyanda za Juu Kusini imefanya semina ya kutoa elimu ya kutambua bidhaa bandia,bidhaa halisi, ushindani wa masoko na kumlinda mlaji kwa Umoja wa Wafanyabiashara wa soko kuu Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Elimu hiyo imetolewa na Mkuu wa Kanda Ofisi ya Tume ya Ushindani (FCC) Nyanda za Juu Kusini Dickson Mbanga.
Mbanga amelitaja lengo la elimu hiyo ni kusimamia ushindani kwa wafanyabiashara wenye uchumi mdogo, kudhibiti bidhaa bandia na kuwatetea watumiaji ili kumwezesha Mfanyabiashara na mwananchi aweze kusitawi katika hali nzuri.
“Bidhaa bandia ni bidhaa ambayo hutumia nembo ya bidhaa nyingine bila ridhaa ya mzalishaji wa bidhaa halisi” amesema Mbanga.
Ameyataja mambo yanayozorotesha ushindani wa kibiashara ni kufanya mikataba isiyo rasmi kama kufunga maduka na kupandisha bei kiholela.
Kwa upande wake Mdhibiti Bidhaa Bandia kutoka Tume ya Ushindani Nyanda za Juu Kusini Anderson Rwiza amezitaja sifa tatu za kutambua bidhaa bandia kuwa ni bidhaa lazima iwe na jina la bidhaa,nembo na mtengenezaji.
Naye Afisa Biashara Mkoa wa Ruvuma Martin Kabalo amewaomba wafanyabiashara waanze taratibu kutambua bidhaa bandia ili kumlinda mlaji na kuepuka madhara mbalimbali ya kiafya kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Masoko ya Manispaa ya Songea Nico Charles amewashauri wafanyabiashara kutumia bidhaa halisi ili kuwaepusha wateja wao na magonjwa mbalimbali kama saratani matatizo ya figo na moyo.
Mfanyabiashara wa soko kuu Raphael Mbilinyi ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha Tume ya Ushindani ili iweze kuwaelimisha kuhusu bidhaa bandia na halisi katika ushindani wa masoko.
Mfanyabiashara wa Soko kuu Jenipha Lucas amesema kutokana na elimu aliyopata hatauza tena bidhaa bandia ili kuepusha madhara kwa walaji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.