Wafanyabiashara wa mazao Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wametakiwa kufuata taratibu zilizopo wakati wa kusafirisha mazao ili kuepuka usumbufu pamoja na adhabu ya kulipa faini pindi watakapokiuka taratibu zilizopo.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura alipozungumza na wafanyabiashara hao ofisjni kwake
" kuna baadhi ya wafanyabiashara hawafuati sheria zilizopo wakati wa kusafirisha mazao kuna baadhi hata leseni zimepita muda wake sasa ili tuweze kwenda sawa lazima tufuate taratibu zilizowekwa'',alisema.
Aidha amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kutoa taarifa pindi wanapogundua wafanyabiashara ambao wanakiuka taratibu hatua ambayo itapelekea kudhibiti upotevu wa mapato.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.