MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema Mkoa wa Ruvuma utawashughulikia wafugaji wote ambao wameingia mkoani umo bila ya kufuata sheria na utaratibu kwani kama Mkoa hawapo tayari kushuhudia migogoro kati ya wakulima na wafugaji
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Mkongo tarafa ya Gulioni katika Wilaya ya Namtumbo alisema wafugaji ambao wameingia mkoani umo bila kufuata sheria warudi walipotoka kwani mkoa utafanya opresheni ya kuwabaini na kuwachukulia sheria
Kanali Thomas alisema Mkoa wa Ruvuma umetenga maeneo ya vitalu kwa ajili ya wafugaji lakini haiwezekani Serikali kuwachimbia maji kwenye vitalu vyao pia amewata wakuu wa Wilaya kutojihusisha kwenye kuwatafutia maji kwani ni wajibu wao kwa mifugo yao
“Kuanzia leo hatutaruhusu kuingiza mifugo mkoa wa Ruvuma mpaka pale tutakapo kamilisha kufanya zoezi la uhakiki wa mifugo iliyopo na kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo navitaka vishirikiane kutekeleza zuio hilo na sisi wananchi tuwe walinzi tuoa taarifa mapema”alisema kanali Thomas
Hata hivyo ameziagiza Halmashauri zote mkoani umo kusimamia vibali na ufuatiliaji kwa wafugaji pia amewasisitiza wananchi kuwa walinzi na kutoa taarifa mapema kabla ya dosali kujitokeza ili wafugaji wasio fuata utaratibu waweze kubainika
Pia ameagiza viongozi vijiji kusimamia sheria na kutenda haki na kwa wale wenyeviti ambao wanahusika na migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuwaingiza wafugaji bila kufuata sheria na wamechukuaa rushwa wachukuliwe hatua za kinidhamu
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.