Wagonjwa 118 wamefanyiwa operesheni ya kuondoa mtoto wa jicho katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma
Daktari wa Macho katika hospitali hiyo Dr.Charles Hinjo amesema madaktari wa macho wa ndani na nje ya nchi wapo mkoani Ruvuma kufanya kazi ya ziada ya kuwahudumia wagonjwa wa macho kwa gharama nafuu.
Amesema kazi hiyo inafanyika kwa siku kumi katika hospitali ya Mkoa Songea ambayo ilianza Novemba 20 na inatarajia kukamilika Novemba 28 mwaka huu.
“Tangu tumeanza kutoa huduma leo ni siku ya nne wagonjwa wa macho 363 wameonwa kati yao, wagonjwa 118 wenye mtoto wa jicho wamefanyiwa operesheni “,alisema.
Hata hivyo Dr.Hinjo amesema lengo ni kuwafanyia operesheni wagonjwa 250 wenye mtoto wa jicho hivyo ametoa rai kwa wananchi mkoani Ruvuma na mikoa jirani kujitokeza kutumia fursa hiyo kupata matibabu ya macho.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.