WAGONJWA 568 wa Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wamepata huduma na kutibiwa na Madaktari bingwa walioletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan .
Madaktari hao walianza kazi katika Mkoa wa Ruvuma Mei 6,2024 na wamehitimisha zoezi hilo Mei 10 katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Madaba Dr.Chacha Wambura amesema ujio wa Madaktari hao umesababisha upatikanaji wa fedha zaidi ya shilingi Milioni mbili kwa wagonjwa waliopata matibabu bila bima.
Hata hivyo Wambura amemshukuru Rais Samia kwa kuleta Madaktari bingwa ambao wameleta chachu kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma na kwa upande wao Madaktari wamejifunza mambo mengi.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Mussa Rashid amesema kupitia zoezi la Madaktari bingwa wamejipanga kuhakikisha wanaboresha utoaji wa huduma za Afya katika hospitali hiyo ambayo pia inapokea wagonjwa wengi kutoka Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.