Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya, hususan kwa mama na mtoto, ambapo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imeanza kutoa huduma ya upasuaji kwa wajawazito wanaopata changamoto wakati wa kujifungua.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Salum Bundalah, huduma hiyo ilianza kutolewa tarehe 21 Februari 2025, na hadi kufikia 13 Machi 2025, jumla ya wajawazito 11 walikuwa wamepata huduma hiyo huku afya zao zikiendelea kuimarika.
Baada ya kuanzishwa kwa huduma hiyo, idadi ya wajawazito wanaohudhuria hospitalini hapo imeongezeka, kwani sasa wana uhakika wa kupata upasuaji iwapo watakumbwa na changamoto wakati wa kujifungua.
Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la Pili, Sinyati Lomnyak Saitabau, ameeleza kuwa huduma hiyo itachangia kupunguza vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
Mmoja wa walionufaika na huduma hiyo, Salome Mwakalinga, amepongeza serikali kwa kuanzisha huduma hiyo, akisema kuwa imepunguza gharama na adha ya kutafuta matibabu mbali, hali ambayo hapo awali ilikuwa inahatarisha maisha ya mama na mtoto.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.