WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha SAUT tawi la Songea waliohitimu Mwaka 2016 hadi 2018 katika fani tofauti wametembelea eneo la Uwekezaji la Silver Land Ndolela Katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Wahitimu hao walitembelea shamba hilo wakiwa wameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile na Mkuu wa Idara ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi Halmashauri ya Madaba Joseph Mrimi.
Moja kati ya wahitimu hao Ernest Anord amesema wemepewa fursa ya kufika kujifunza katika eneo la uwekezaji wa mbegu za mazao mbalimbali.
Amesema wameona eneo la uwekezaji kupitia teknolojia ya umwagiliaji lenye ukubwa wa hekta 500 linalowekezwa katika mbegu za viazi mviringo, Alizeti na Maharage aina 72 za Mbegu ya ngano.
Meneja wa Kampuni hiyo ya Silver Land Ndolela Christian Kihindo amesema Kampuni hiyo kwa mara ya kwanza walianza kulima Mahindi ya chakula,ngano pamoja na Soya katika msimu wa Mwaka 2016/2017.
Kihindo amesema kwa sasa wawekezaji hao Mbegu wanauza ,mbegu katika kampuni za Tanzania na nchi ya Italia.
Amesema wawekezaji hao wanalima mara mbili kwa mwaka kwa umwagiliaji kupitia umeme wao uliotegwa kupitia maporomoko ya Mto Ruhuhu
Kampuni ya Silver Land Ndolela ina wafanyakazi 150 wenye ajira ya kudumu na ajira ya muda mfupi ni zaidi ya 600.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.