AFISA Biashara wa Mkoa wa Ruvuma Joseph Martin amefungua kikao cha wauza pembejeo za Kilimo kupitia mradi wa Wakala Digital.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Anglican Manispaa ya Songea amesema mradi wa Digital ambao unafadhiliwa na Shirika la AGRA na kutekelezwa kupitia taasisi mbili ambazo ni RUCODIA na QUINCEWOOD kuhakikisha malengo makuu matatu.
Martini ameyataja malengo hayo ikiwemo kuwa na mfumo wa kidigitali ambao utasaidia wasambazaji wa pembejeo wakubwa wataweza kusimamia biashara vizuri,kuboresha mfumo wa utunzaji kumbukumbu pamoja na kuimarisha njia ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo katika maeneo ya vijijini kwa kuboresha uwezo wa wauzaji pembejeo za kilimo wakubwa walio mjini.
“Mkoa wa Ruvuma jumla ya wauzaji wa pembejeo wapatao 75 wameanza kutumia mfumo wa wakala digitali katika kujisajili na kusajili bidhaa”.
Hata hivyo amesema wauzaji wa pembejeo walikuwa na hofu kuhusu usalama wa taarifa za biashara zao zinapowekwa kwenye mfumo wa wakala wa dijitali.
“Niwahakikishie kuwa taarifa zenu ziko salama,kila mmoja ataweza kupata taarifa zake mwenyewebila kuingiliana na mtu mwingine”.
Meneja wa Mradi huo Filbet Misigiro amewaomba wauzaji wa Pembejeo kutumia mfumo huo ambao unasaidia kudhibiti Pembejeo feki ili kuwasaidia kupata Pembejeo bora na kuwasaidia wakulima kutopata hasara.
Amesema Mfumo huo kwa wauzaji wapembejeo utawaongoza katika uagizaji wa pembejeo na kupata takwimu sahihi pamoja na Mauzo ya kila siku ,Mwezi pamoja na Mwaka.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Februari 2,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.