WAKULIMA wa mahindi mkoani Ruvuma,wamekumbushwa umuhimu wa kufuatilia maendeleo ya mazao yao mashambani na kuhakikisha wanavuna mazao yaliyokomaa ili kupata soko la uhakika.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Kanda ya Songea Zenobius Kahere, wakati akizungumzia maandalizi ya ununuzi wa mahindi katika msimu wa kilimo 2024/2025 ofisini kwake mjini Songea.
Amesema,hatua hiyo itawezesha NFRA kupata nafaka bora kwa ajili ya akiba ya chakula kwa wananchi watakaopatwa na upungufu wa chakula katika maeneo yao.
Kwa mujibu wa Meneja huyo,katika msimu wa mwaka huu NFRA itanunua mahindi kwa kuwahusisha wakulima wakubwa,wafanya biashara wakubwa na wakulima wadogo.
Amebainisha kuwa,wakulima wakubwa waliokusudiwa katika mpango huo ni wakulima wanaoanza na hekari 100 na wenye uwezo wa kuuza tani 200 na kuendelea.
“Kwa upande wa wafanya biashara ni wale wenye uwezo wa kununua mahindi kutoka kwa wakulima kuanzia tani 2,000 hadi 5,000”.
Amevitaja,vigezo vilivyowekwa kwa wakulima wakubwa watakaotaka kuuza mahindi kwa Serikali kuwa ni lazima atoke kwenye Halmashauri anayofanyia shughuli zake za kilimo ili NFRA iweze kumpa mkataba wa kuuza mazao yake kama mkulima na siyo vinginevyo.
Hata hivyo amesema,wafanyabiashara wakubwa watalazimika kuwa na barua ya utambulisho kutoka kwa Halmashauri ya wilaya wanakofanyia biashara zao ili muda utakapofika wa kuanza kununu nafaka iwe rahisi kwa NFRA kuweka usimamizi mzuri wa upatikanaji wa nafaka hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.