• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAKANDARASI Ruvuma washauriwa kutekeleza miradi kwa uadilifu na ubora

Imewekwa kuanzia tarehe: January 27th, 2022

WAKANDARASI wa miradi ya maji mkoani Ruvuma, wametakiwa kutekeleza miradi  waliyopewa kwa uadilifu na ubora wa hali ya juu ili miradi hiyo iweze kumaliza kero ya upatikanji wa huduma  ya maji kwa wananchi.

Hayo yamesemwa  na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, katika Hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Nyasa Kanali  Raban Thomas, wakati wa utiaji saini wa mikataba  mitano ya ujenzi wa miradi ya maji  inayotarajiwa kutekelezwa katika wilaya  nne kati ya tano za mkoa huo.

Jenerali Ibuge, amewataka wakandarasi hao kutumia  vizuri nafasi hiyo kuonyesha uwezo wao kwa kujenga miradi yenye ubora ili kuipa serikali imani na kuendelea kuwaamini wakandarasi wa ndani kwa kuwapa miradi mingine.

Mkuu wa mkoa, amewaagiza wahandisi wa miradi ya maji mkoani humo,kusimamia vizuri kazi hiyo ili iwe na ubora na kuhakikisha wakandarasi wanalipwa kwa wakati mara baada ya kukamilisha kazi walizopewa.

Brigedia Jenerali Ibuge,ametaka kuwepo ushirikishwaji wa viongozi  wa ngazi ya wilaya na mkoa kwenye miradi hiyo, kwani jambo hilo linaweza kuleta tija katika utekelezaji wa miradi ya maji na miradi mingine ya maendeleo mkoani humo.

Ametoa wito kwa wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za wilaya ambazo miradi hiyo inakwenda kutekelezwa,kuwapa ushirikiano wakandarasi hao ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri  na kutambulisha miradi hiyo kwa wananchi  kwa kuwa wao ndiyo walinzi wanaoishi katika mazingira ya miundombinu hiyo.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma Stephen Ndaki alisema,mikataba hiyo ni muhimu kwa sababu mahitaji ya maji kwa wananchi na ustawi wa nchi yetu ni makubwa na kuwataka wakandarasi kwenda kutekeleza miradi  kwa wakati na kulingana mikataba iliyopo.

Amewataka kutanguliza uzalendo, na kutekeleza miradi hiyo kwa weledi wa hali ya juu,ubora unaotakiwa na  ilingane na fedha zilizotolewa na Serikali  ili  kuleta ufanisi na tija kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma ambao baada ya mikataba hiyo wana matarajio makubwa ya kupata maji kwa haraka.

“maana ya ufanisi  ni pale mradi unapotekelezwa na kutoa matokeo mazuri na msipofikia ufanisi ni nadra sana kupata matokeo  mazuri ya miradi husika”alisema Ndaki.

Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini Ruwasa mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga alisema, kwa mwaka wa fedha 2021  Ruwasa mkoa wa Ruvuma imetengewa jumla ya Sh.11,914,448,813.00.

Alisema, fedha hizo zinalenga kuhakikisha  miradi yote waliyoipanga katika mwaka  2021/2022 inatekelezwa na kutimiza dhamira ya Serikali ya kumtua mama ndoo kichwani.


Kwa mujibu wa Ganshonga,miradi ambayo mikataba yake imesainiwa itagharimu jumla ya Sh.3,806,744,369.18 fedha zilizotolewa na Serikali Kuu kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19 na itatekelezwa kwa siku 120 na miradi itakayotekelezwa kwa vyanzo vingine  muda wake ni siku 180.


Alisema,miradi hiyo inakwenda kutekelezwa kutokana na vyanzo mbalimbali vya fedha ambapo miradi 3 ni ya fedha za Mpango wa maendeleo kwa  Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19 na miradi 2 itatekelezwa kwa fedha za vyanzo vingine(NWF,PBR,GoT na PFR).


Alisema,miradi ambayo imepangwa kutekelezwa imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni miradi ambayo taratibu za manunuzi zinafanyika ngazi ya Wizara na miradi ambayo taratibu za manunuzi zinafanyika ngazi ya Mkoa.


Ganshonga alisema, miradi yote ilikuwa katika hatua mbalimbali za kukamilisha usanifu na uandaaji wa taarifa na nyaraka za zabuni  kabla ya kuitangaza kupitia mfumo wa manunuzi ya umma ili kuwapata wakandarasi wenye sifa na kutekeleza kazi za ujenzi wa miradi hiyo.

Alisema,katika miradi ambayo utaratibu wa manunuzi ulikuwa unafanywa na Ruwasa mkoa,jumla ya miradi 5 kati ya 15 taratibu zake za zimekamilika.


Alisema,Ruwasa mkoa inaendelea kutekeleza miradi mingine 17 ambayo ipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji kwa kutumia wataalam wa ndani kwa mfumo wa force Akaunti.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.