MKUU wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Simon Chacha,amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya barabara wilayani humo kuzitendea haki fedha zinazotolewa na Serikali kwa kujenga miradi yenye viwango itakayosukuma na kuharakisha shughuli za maendeleokwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Chacha amesema hayo,wakati akizungumza na watumishi wa TARURA na wakandarasi waliopata kazi za ujenzi wa miradi ya barabara zinazosimamiwa na wakala wa barabara za mijini na vijijini(TARURA)wilayani humo.
Chacha,amewaeleza wakandarasi hao kutekeleza kazi zilizoko kwenye mikataba waliyoingia na Serikali kupitia Tarura,kuwa wazalendo kwa nchi yao na kujenga miradi yenye viwango ambayo itachochea na kuharakikisha kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja,wilaya na Taifa.
“Nendeni mkapige kambi kwenye maeneo ya miradi ili mpate muda mwingi utakaowawezesha kukamilisha kazi mlizopewa kwa wakati, wananchi wana matarajio makubwa na nyinyi, epukeni kuwa na visingizio vinavyoweza kuchelewesha ujenzi wa miradi”alisema Chacha.
Meneja wa TARURA wilaya ya Tunduru Silvanus Ngonyani amesema,kwa mwaka wa fedha 2024/2025 TARURA Wilaya ya Tunduru,imeidhinishiwa Sh.bilioni 4,110,783,784.47 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya fedha.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya kupambana na Kuzuia Rushwa(TAKUKU)Wilayani humo George Njoholo, amewataka wakandarasi kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango ili iendane na gharama halisi ya fedha zilizotolewa na Serikali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.