• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAKAZI Matepwende Namtumbo waiomba TARURA kukamilisha daraja

Imewekwa kuanzia tarehe: June 10th, 2023

KILIO cha muda mrefu cha wakazi wa kijiji cha Matepwende na kitongoji za Zanzibar  wilayani Namtumbo, kukosa mawasiliano ya uhakika kutokana na mto Kotoka unaotenganisha maeneo hayo kujaa maji kimepata majibu baada ya Wakala wa barabara za mijini na vijijini(TARURA)kuanza ujenzi wa daraja la kisasa katika eneo hilo.

Mradi huo umetengewa jumla ya Sh.milioni  638 ambazo zitatumika kujenga daraja lenye urefu wa mita tano,makalavati matatu na kazi ya kufungua barabara mpya yenye urefu wa kilomita 34 kazi inayotarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu.

Mtimba alisema,mradi huo unalenga kurahisisha mawasiliano na shughuli za usafiri na usafirishaji wa bidhaa ikiwemo mazao kutoka shambani kwenda sokoni na kuchochea  ukuaji wa uchumi.

Alisema,kwa sasa wananchi hasa wakulima wanapata shida kubwa kupita katika mto huo  kutokana na ubovu wa barabara,lakini ujenzi wa daraja utakapokamilika changamoto hizo zitamalizika na hata kupungua kwa gharama za usafirishaji wa bidhaa na mazao.

Aidha alisema,ujenzi wa daraja na ufunguzi wa barabara hiyo ni sehemu ya mkakati wa TARURA kufungua barabara hadi kwenye maeneo yenye uzalishaji mkubwa na kufika kusiko fikika ambapo  Tarura imejipanga kuendelea kufungua barabara mpya katika maeneo mbalimbali wilayani Namtumbo.

Amewaomba wananchi,kuhakikisha wanatunza daraja hilo ili liweze kudumu kwa muda mrefu na kuepuka kufanya vitendo vinavyoweza kuchelewa kukamilika kwa mradi huo mkubwa unaotekelezwa kwa faida yao.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Matepwende,wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa kujenga daraja katika mto huo ambao kwa muda mrefu umekuwa sehemu ya kukithiri kwa umaskini kwenye familia zao.

Abbas Yasin ameiomba serikali kupitia TARURA,kuharakisha ujenzi wa daraja na ufunguzi wa barabara hiyo ili waweze kuitumia kusafirisha mazao hasa msimu huu wa mavuno ulianza tangu mwezi Mei.

Alisema,barabara hiyo ni kero kubwa na ndiyo iliyosababisha wao kuwa na kiwango kikubwa cha umaskini kwani licha ya kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula na biashara,lakini wameshindwa kupiga hatua na kunufaika na kazi za kilimo kwa sababu ya kushindwa kusafirisha mazao yao hadi sokoni kutokana na ubovu na kupanda kwa gharama za usafirishaji.

Alieleza kuwa,kutokana na hali hiyo wafanyabiashara wasiokuwa na huruma wanatumia nafasi ya kwenda moja kwa moja mashambani na kununua mazao kwa bei ndogo isiyolingana na uzalishaji mashambani.

Mkulima wa kitongoji cha Zanzibar Yakin Kanyalo alisema,kukosekana kwa daraja katika mto Kotoko na ubovu wa barabara hiyo unasababisha wanawake wajawazito,wazee na watoto kushindwa kufika kwa wakati kwenye vituo vya afya.

Aliongeza kuwa,wapo wananchi waliopoteza maisha kwa kushindwa kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya pindi wanapopatwa na ugonjwa wa ghafla,mama wajawazito kujifungulia njiani  wakati wakipelekwa kupata huduma kituo cha Afya Namtumbo au Hospitali ya wilaya

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • SEKONDARI ya Dkt.Samia alama ya maendeleo Namtumbo

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.