MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema wakazi 1,149,867 katika Mkoa wa Ruvuma wanapata maji safi na salama hadi kufikia Oktoba 2020.Akitoa taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma kwa Waziri Mlkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi mkoani humu,Mndeme amesema idadi hiyo ya watu ni sawa na asilimia 63.9 ambapo idadi ya watu wanaopata maji vijijini ni sawa na asilimia 61.6 wakati wakazi wa mijini ni asilimia 66.4.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema uboreshaji wa huduma za maji mijini na vijini hadi kufikia Oktoba mwaka jana Mkoa ulitekeleza miradi 29 ya ukarabati na upanuzi iliyogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.168 kupitia program ya lipa kwa matokeo(PBR) ambapo jumla ya miradi 19 imekamilika na miradi kumi inaendelea kutekelezwa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma miradi 33 ya programu ya lipa kwa matokeo ipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Januari 11,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.