MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania wametoa mafunzo ya Bima kwa Vikundi vya wakulima na Wafugaji wa Mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza katika uzinduzi wa Mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Jeremia Sendoro amesema mafunzo hayo yameletwa Mkoa wa Ruvuma kwasababu ni Mkoa wa kilimo na ufugaji wa Samaki kwa Wingi.
wameona umuhimu wa kutoa Elimu na kuwajengea uelewa.
“Bima ya kilimo na Ufugaji inatusaidia pale tunapopata hasara katika Mazao yanapokuwa Shambani, kama utatokea ukame au mvua za mawe pamoja na mifugo kufa kwa magonjwa au wanapokuwa marishoni Bima inatoa fidia ”.
Sendoro ametoa rai kwa Wakulima na Wafungaji kufuatia mafunzo hayo kufuata yale waliyopata kutoka kwa wataalamu na kuyafanyia kazi pamoja na kuwa na kilimo chenye tija na kuwa mabalozi kwa wengine ili kuepuka hasara katika kilimo na Ufugaji.
“kuna wenzetu wa Bodi ya Kilimo,Nafaka na Mazoa mchanganyiko Soya na mazao mengine katika mikataba yao walitaka Bima ya Kilimo utekelezaji ulikuwa mgumu kwasababu ya kukosa Bima”.
Hata hivyo amesema Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania wemekuja wakati mzuri wa mavuno ikiwemo Soya, Maharage ,Mahindi na Octoba ni mwezi wa mavuno ya Korosho pamoja na Novemba kuandaa Mashamba hivyo mafunzo hayo yametolewa wakati sahihi na kwawatakaopenda kilimo cha Mkataba na Pamoja wataalamu watasimamia kilimo hicho.
Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Kanda ya Nyanda za Kusini Salum Yungwa amesema lengo la Mafunzo hayo Mkoani Ruvuma kutoa Elimu ya Bima ya Kilimo kwa wakulima ambao wanaoathirika na majanga mbalimbali yanayoweza kutokea wakati mazao yakiwa Shambani,Njiani au Kwenye ghara.
Yugwa amesema wametoa Semina kwa wakulima na wafugaji mara baada ya kuona Mkoa wa Ruvuma ni moja kati ya Mikoa iliyojikita katika uzalishaji wa Kilimo na Ufugaji kwa wingi.
“Leo tumetoa uelewa kwa Wanaruvuma ili waelewe Umuhimu wa Bima na kujikinga na majanga ambayo yanaweza kujitokeza na fidia itapatikana na kutopata hasara ”.
Amesema kupitia Mafunzo hayo yaliyotolewa Wakulima na wafugaji wamepata Hamasa na wapo tayari kutumia Bima katika Kilimo na Ufugaji kwa kuepuka kupata hasara zitakazojitokeza mara kwa mara.
Moja kati ya Washiriki wa Mafunzo hayo Heriety Komba amesema kuna baadhi ya wakulima bado hawakujua umuhimu wa Bima na mara kwa mara wamepata majanga katika Kilimo na Ufugaji hivyo kupitia Semina hiyo wamepata uelewa na watafanyia kazi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde na Jackson Mbano
Kutoka Kitengo cha Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
April 28,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.