Wakulima mkoani Ruvuma waingiza zaidi ya shilingi bilioni 644 baada kuuza mazao ya kahawa na korosho kwenye misimu mitano mfululizo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema Mkoa wa Ruvuma kwa vipindi vya misimu ya kilimo mitano mfululizo kutoka msimu wa kilimo 2017/2018 hadi kufikia msimu 2020/2021 jumla ya kilo 77,664,927.75 za kahawa zilikusanywa.
Amesema kilo hizo ziliuzwa kwa watani wa bei sh. 4,638 na kuwapatia wakulima wa kahawa zaidi ya shilingi bilioni 353.
Amebainisha kuwa kati ya fedha hizo,msimu wa mwaka 2016/2017 zilinunuliwa kilo 15,393.500 zilizowaingizia wakulima zaidi ya shilingi bilioni 66 na kwamba msimu wa 2017/2018 zilinunuliwa kilo 20,162,900 na kuwaingizia wakulima zaidi ya shilingi bilioni 74.
Kwa mujibu wa Kanali Thomas katika msimu wa mwaka 2018/2019 zilinunuliwa kilo 15,675,100 zilizowaingiza wakulima zaidi ya shilingi bilioni 64,msimu wa mwaka 2019/2022 zilinunuliwa kilo 12,676,844 zilizowaingiza wakulima zaidi ya shilingi bilioni 50 na kwamba mwaka 2020/2021 zilinunuliwa kilo 15,756,583.75 na kuwaingiza wakulima zaidi ya shilingi bilioni 97.
Akizungumzia kuhusu zao la korosho,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema kwa msimu wa masoko 2022/2023 minada ilianza tarehe 10/11/2022.
“Hadi kufikia tarehe 24/12/2022 Mkoa ulikusanya jumla ya kilo 6,123,688 za Korosho zenye thamani ya shilingi bilioni . 11,406,932,180 ambazo ziliuzwa kwa wastani wa bei sh. 1852.33 kwa kilo’’,alisema RC Thomas.
Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma kwa vipindi vya misimu ya kilimo minne mfululizo kutoka msimu wa kilimo 2017/2018 hadi kufikia msimu 2020/2021 jumla ya kilo 104,819,739.00 za Korosho zilikusanywa na kuuzwa kwa wastani wa bei sh. 2,801 na kuwapatia wakulima zaidi ya shilingi bilioni 291.
Amesema Serikali kupitia vyama vya Ushirika imetekeleza na inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo usimamizi wa uendelezaji wa ujenzi wa kiwanda cha vifungashio cha Chama Kikuu SONAMCU wilayani Namtumbo na ukarabati wa maghala matano kati ya saba ya Chama Kikuu cha Ushirika Mbinga MBIFACU.
Miradi mingine inayotekelezwa na ushirika ameitaja kuwa ni Ukarabati wa hoteli ya MBICU mjini Mbinga,usimamzi na uendelezaji wa Mradi wa kiuchumi wa shamba la kahawa la MBIFACU,ujenzi wa Mradi wa shule ya Sekondari ya Mahenge AMCOS na Ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao ya wakulima la chama cha Msingi Kimuli na Namitili (AMCOS) wilayani Mbinga.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma katika msimu wa 2022/2023 unaendelea kutekeleza mpango wa kilimo cha mazao kupitia kilimo cha pamoja (block Farming),ikiwa na lengo la kuongeza uzalishaji na kuweza kumpatia tija mkulima.
Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Februari 14,2023
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.