WADAU wa maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamewataka viongozi kuimarisha mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umeonesha mafanikio makubwa kwa wakulima.
Ally Lyuma Mkazi wa Namtumbo amesema ipo haja ya uongozi wa Halmashauri ya Namtumbo kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani Kwa kuwa mfumo huo una manufaa Kwa wakulima wa kipato Cha chini.
Meneja wa Chama Cha Msingi (AMCOS) Naikesi Lukas Sesilius amesema wakulima wa AMCOS hiyo wanaishukuru serikali Kwa kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani Kwa kuwa wakulima wana uhakika wa soko la mazao yao.
Diwani wa Kata ya Likuyu Mheshimiwa Kassim Gunda amewataja wanaolalamikia mfumo wa stakabadhi ghalani kuwa haufai sio wakulima ni madalali ambao waliozoea Kununua mazao Kwa wakulima kwa bei ya chini na kwenda kuuza kwa bei ya juu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Juma Pandu amewashauri wataalamu wa kilimo kuimarisha zaidi mfumo wa stakabadhi ya ghala Kwa kuwa una ndiyo mkombozi wa wakulima .
.Takwimu za uuzaji mazao ya wakulima kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani mkoani Ruvuma kwa kipindi cha mwaka 2023/2024 zinaonesha wakulima waliingiza mabilioni ya fedha.
Kulingana na takwimu hizo katika zao la mbaazi wakulima waliingiza zaidi ya bilioni 18 baada ya kuuza kilo 9,298,347 za mbaazi na zao la ufuta liliwaingizia zaidi ya bilioni 31 baada ya kuuza kilo 8,621,162.
Kwa mujibu wa takwimu hizo zao la korosho liliwaingizia zaidi ya bilioni 40 baada ya kuuza kilo 26,062,323 na zao la soya liliwaingizia zaidi ya bilioni nne baada ya kuuza kilo 5,023,309.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.