wakulima wa Kata ya Kilagano Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kupeleka minada ya mazao moja kwa moja vijijini kwa wakulima wanaozalisha mazao.
Walikuwa wanazungumza kwenye mnada wa ufuta uliofanyika katika kijiji cha Mgazini Kata ya Kilagano ambapo wakulima wameweza kuuza tani 272 za ufuta kwa bei ya jumla ya shilingi 3,773 kwa kilo moja kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.
Wakulima hao wamesema wameridhika na bei ya ufuta kupitia mfumo ambapo wamesisitiza bei hiyo itawahamasisha msimu ujao kuongeza uzalishaji wa zao la ufuta na mazao mengine kwa kuwa mfumo unatoa bei yenye tija kwa mkulima.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.