• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAKULIMA Tunduru wauza kilo 308,774 za korosho

Imewekwa kuanzia tarehe: January 14th, 2023

JUMLA ya kilo 308,774 za korosho  kutoka vyama vya msingi vya ushirika vinavyosimamiwa na Chama Kikuu cha ushirika wilaya ya Tunduru (Tamcu Ltd), zimeuzwa katika mnada wa 10 uliofanyika katika ghala la TAMCU Tunduru mjini.

Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika(Tamcu)wilayani Tunduru Imani Kalembo alisema, katika mnada huo kampuni moja  ya RV Export Ltd ndiyo imejitokeza kuomba kununua ambapo korosho daraja la pili  ziliuzwa kilo 151,440 kwa bei ya sh.1,340 kwa kilo moja na daraja la kwanza zimeuzwa kilo 157,334 kwa sh.1,600.

Alisema,hadi sasa Chama Kikuu kimeshafanya minada 9 na jumla ya tani 14,380 zenye thamani ya Sh.bilioni  25 zimekusanywa na kuuzwa  kwa makampuni mbalimbali.

Hata hivyo alieleza kuwa,kiasi hicho cha korosho zilizozalishwa katika msimu 2022/2023 ni nusu ya uzalishaji msimu wa mwaka 2021/2022 kwani katika msimu uliopita wakulima walifanikiwa kuzalisha na kuuza zaidi ya tani 25,000.

Kalembo,amewaasa wakulima ambao bado wana korosho majumbani,kuhakikisha wanapeleka kwenye vyama vyao vya msingi(Amcos) kwa ajili ya kuuza ili kuwahi mnada wa mwisho utakaofanyika wiki ijayo.

Aidha,amewataka kufanya palizi ya mashamba yao na kutumia fedha wanazopata kununua pembejeo za ruzuku zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita,na kuepuka kutumia kwenye mambo ya anasa jambo linaloweza kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

Makamu mwenyekiti wa Tamcu James Chipojola alisema,uzalishaji mdogo wa korosho katika msimu wa mwaka huu umeathiriwa sana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo mvua za masika ziliwahi kunyesha  na hivyo kuathiri sana uzalishaji na kupunguza ubora wa korosho.

Chipojola,amewashauri  wakulima ambao ni wanachama wa Tamcu, kuanza kulima mazao mengine ya biashara kama vile ufuta,mbaazi,soya, na alizeti ili kujiongezea kipato,badala ya kutegemea zao moja tu la korosho ambalo kwa sasa linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ya bei.

Naye Afisa ushirika wa wilaya hiyo George Bisani alisema, katika msimu wa 2022/2023  malengo yalikuwa kuzalisha tani 30,000 lakini hawawezi kufikia kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo mashambani.

Bisani,amewaomba wakulima kutokata tamaa kutokana na changamoto zilizojitokeza katika msimu huu,bali waendelee kufanya maandalizi ya msimu mpya kwa kupalilia mashamba yao na kufuata ushauri  wa wataalam wa kilimo.

Mmoja wa wakulima  wa zao hilo Issa Lada,ameiomba serikali kusimamia bei ya korosho kwani  wakulima wanatumia gharama kubwa katika uzalishaji,lakini bei zinazotolewa na makampuni yanayonunua korosho ni ndogo na hailingani na gharama za uzalishaji wake.

Alisema,kama serikali itajipanga na  kusimamia vizuri suala ya bei kwa zao la korosho uchumi wa wilaya hiyo utakuwa mkubwa na wakulima watapata fedha nyingi  na kuongeza uzalishaji mashambani.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.