Serikali Mkoani Ruvuma imewahakikishia wakulima na wazalishaji wa zao kahawa katika Wilaya za Mbinga na Nyasa, kupata masoko ya uhakika ya moja kwa moja ya zao hilo katika kampuni kutoka Mataifa ya Urusi, China na Nchi za Kiarabu (Dubai) kkuanzia katika msimu huu wa kilimo.
Mbunge wa Mbinga Mjini Mheshimiwa Jonas Mbunda ametoa taarifa hizo njema kwa wakulima katika kikao cha wadau wa zao la Kahawa kilichoshirikisha Wilaya hizo mbili za Mkoa wa Ruvuma ambacho kimechofanyika katika ukumbi wa Oddo Mwisho mjini Mbinga.
Naye Mkurugenzi wa Halmashuri ya Mji wa Mbinga Bi Grace Quintine katika kikao hicho amewatambulisha wageni wanunuzi wa zao hilo kutoka nchi za Kiarabu ( Dubai ),Urusi na China, ambapo amesema wageni hao wamepatikana kwa jitihada za waheshimiwa wabunge Jonas Mbunda na Mbunge viti maalum Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa i Jackline Msongozi ambao wameahidi kuendelea kutafuta masoko kwa wakulima hapa nchini hususani katika Mkoa wa Ruvuma katika zao la Kahawa.
Wageni hao wameahidi kununua kahawa ya Mbinga ambayo wamesema hivi sasa inahitajika kwenye soko la dunia kwa kuwa inalimwa bila kutumia kemikali i.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.