Wakulima wa Mkoa wa RUVUMA wametakiwa kuchangamkia fursa ya kilimo cha kahawa kwasababu maeneo mengi ndani ya Mkoa yanafaa kwa kilimo cha kahawa ambacho kitainua uchumi wao.
Wito huo umetolewa na mtaalam wa kilimo Bw Victa Akulumuka kutoka kituo cha utafiti wa zao la kahawa TaCRI cha Ugano Mbinga katika maonesho ya nanenane ngazi ya Mkoa wa Ruvuma yanayofanyika viwanja wa Msamala mjini Songea.
Akalumuka amesema wakulima wanatakiwa kuchangamkia fursa ya kulima zao la kahawa kwakuwa zao la kahawa linaonekana kustawi katika maeneo mengi ndani ya mkoa na kilimo ambacho kitainua uchumumi wao na Taifa.
Amewataka wakulima kuzingatia amri kumi za kilimo cha kahawa ambazo zinasaidia katika kustawisha zao la kahawa ambazo zitatoa matokeo chanya na kuongeza uzalishaji wenye tija kwa wakulima .
Amezitaja amri za kilimo bora cha kahawa kuwa ni kukatia matawi,kutumia mbolea,kupulizia madawa kwa wakati,kupalilia nakuondoa machipukizi Pamoja na kupanda miti kwa ajili ya kutunza ubaridi katika shamba.
Aidha amesema endapo wakulima watafuatilia na kusimamia na kufuatilia kilimo cha kahawa mkulima anaweza kuvuna kilo tatu kwa shina moja,ambapo kwa hekali moja mkulima anaweza kuvuna kilo Zaidi ya 1500 kutokana na shamba lenye ukubwa wa hekali moja ambapo hupandwa miche 540
Ameomba maafisa ugani wa wa Halmashauri mkoani Ruvuma kutoa elimu juu ya usimamizi na ufuatiliaji wa zao la kahawa kwalengo la kuwasaidia wakulima kupata mavuno mengi na kunufaika na kilimo cha kahawa ambacho ni miongoni mwa mazao ya kimkakati Nchini.
“Ukichukulia miaka 10 iliyopita eneo la Liganga wilayani Songea kwenye shamba la kahawa la AVIV palikuwa hapajulikani kama panafaa kulima zao la kahawa lakini kampuni ya AVIV imeonesha mfano kwamba ardhi ya Ruvuma inafaa kwa kilimo cha kahawa”,alisema Akalumuka.
Utafiti umebaini kuwa mkoa wa Ruvuma una maeneo mengi ambayo yanafaa kwa kilimo cha zao la kahawa ikiwemo Wilaya Mbinga na wilaya ya Songea katika kata za Liganga,Mbingamhalule,Kizuka,Parangu LItisha,Ndongosi na Mpitimbi na Madaba.
Kituo cha utafiti wa zao la kahawa TaCRI kinatoa huduma ya miche bure kwa wakulima wote na utaalama wa kulima zao la kahawa unapatika kutoka kwa maafisa ugani.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 8,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.