Afisa Kilimo wa Chama Kikuu cha Ushirika wilayani Tunduru(TAMCU)Grace Evody,akitoa elimu ya kilimo bora cha korosho na mazao mengine ya kimkakati jana kwa wakulima wa kijiji cha Luginga wilayani humo kama mkakati wa chama hicho wa kuongeza uzalishaji wa korosho bora zitakazopata soko la uhakika.
Serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania,inatarajia kuanza kusajili wakulima wa korosho ili kuwatambua na kupata idadi kamili ya wenye sifa kabla ya kupata pembejeo za ruzuku kwa msimu wa kilimo 2024/2025 katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Hatua hiyo inalenga kurahisisha uendeshaji wa zao la korosho,kupata idadi ya pembejeo zinazotakiwa kwenda kwa wakulima,kupunguza upotevu wa pembejeo na kuondoa adha kwa wakulima kutafuta na kuuzia pembejeo hizo kwa bei kubwa.
Hayo yamesemwa na Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Tanzania Tawi la Tunduru Samwel Kambona,alipokuwa akizungumza na wakulima, wajumbe wa bodi ya TAMCU pamoja na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS)mjini Tunduru.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.