• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAKULIMA washauriwa kuuza ufuta kupitai stakabadhi ghalani

Imewekwa kuanzia tarehe: June 26th, 2022

WAKULIMA wa zao la ufuta katika kijiji cha Molandi kata ya Marumba wilayani Tunduru,wamehamasishwa kuendelea kuuza ufuta wao  kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani na kuzingatia ubora ili waweze kupata fedha nyingi kutokana na zao hilo kuwa na soko kubwa Duniani.

Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro baada ya kutembelea zoezi la kukusanya ufuta wa wakulima katika ghala ya kijiji cha  Molandi wilayani humo.

Amewataka wakulima,kuendelea kuzalisha kwa wingi kwa kuwa mahitaji ya zao hilo kwa sasa ni makubwa ikilinganisha na siku za nyuma kutokana na vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukreni ambapo Mataifa mengi yanahitaji zao hilo.

“nimefanya ziara ya kukagua zoezi zima la upokeaji wa ufuta kwenye ghala la kijiji cha ambao unauzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani, nawaomba sana wananchi waendelee kukusanya ufuta wao na hawauzi nje ya mfumo huo ili waweze kunufaika na  kazi wanayoifanya”alisema Mtatiro.

Aidha Mtatiro,amewaagiza viongozi wa serikali ya kijiji na kata kuhamasisha wananchi waokuchangia fedha na michango mingine kwa ajili ya ujenzi wa ghala kubwa,badala ya kuendelea kutumia ghala lililopo ambalo ni dogo na limeanza kuchakaa.

Amewataka viongozi hao kuwa wabunifu kwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato na sio kutegemea michango ya viongozi na Serikali kwa kuwa tabia hiyo inaweza  washindwe kufanikisha na kutekeleza mipango yao ya maendeleo.

“mimi sishindwi kuwaletea mifuko ya saruji ili kuendelea na ujenzi wa ghala lenu,lakini nahitaji mniletee mpango kazi wenu unaoonyesha  mnahitaji nini,hii ni mara ya tatu nakuja kwenye ghala hili na naweza kurudi tena mara ya nne,sasa kwa utaratibu huu mlionayo hamtaweza kulijenga”alisema Mtatiro.

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya alisema,zaidi ya  tani elfu ishirini na tano(925,000) ya  Dawa ya kupulizia korosho(Salphur)zimeanza kuwasili na kusambazwa kwa wakulima katika  maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Hata hivyo alisema, dawa hizo haziwezi kutosheleza kwa wakulima wote na kuwataka kuanza maandalizi ya msimu mpya kwa kununua  Dawa kwa ajili ya mashamba yao huku wakisubiri utaratibu wa kupata viuatilifu vinavyotolewa na Serikali.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho  Said Manjolo alisema,wakulima wengi wanashindwa kuleta mazao yao kutokana na changamoto ya ghala ambalo kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa ufuta limekuwa dogo.

Ameiomba Serikali kupitia Halmashauri ya  wilaya Tunduru,kuwasaidia kukamilisha ujenzi wa ghala jipya  ambalo ujenzi wake ulianza tangu mwaka jana, lakini wameshindwa kuendelea kutokana na kukosa fedha ili wananchi wasiangaike kuhamisha mazao yao kupeleka maeneo mengine.

Manjolo, ameipongeza serikali kwa kusimamia na kuboresha mfumo wa uuzaji wa zao la ufuta kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umeanza kuleta faida kubwa kwa wakulima.

Alisema, kwa sasa bei ya ufuta imeongezeka kutoka Sh.3000 katika mnada wa kwanza  hadi kufikia Sh.3,040 bei ambayo haijawahi kutokea tangu waanze kulima zao hilo katika kijiji hicho.

Alisema,matarajio ya uzalishaji wa zao hilo  mwaka huu ni makubwa zaidi kutokana na wakulima wengi kujitokeza kulima zao hila la biashara ambapo wanatarajia kuuza zaidi ya tani mia nne mwaka huu.

Mkulima wa zao hilo Said Hassan, ameishukuru na kuipongeza serikali kwa kuhamasisha,kuwapatia pembejeo kwa wakati na kuhakikisha upatikanaji wa soko la uhakika la zao hilo.

“sisi wakulima tunaishukuru sana serikali yetu ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Hassan kwa kutuhamasisha,kutupa elimu na mbegu  na kuweka mazingira mazuri ya soko la ufuta”alisema.

Alisema,kutokana na mazingira mazuri hasa soko la uhakika ndiyo maana wananchi wengi wamehamasika kulima zao hilo na kuachana na kilimo cha baadhi ya mazao  mengine ya biashara ambayo yalikuwa na changamoto nyingi katika uzalishaji wake.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBUNGE Kawawa aleta neema Namtumbo

    May 11, 2025
  • KIONGOZI Mwenge wa uhuru ashiriki upandaji miti Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru waweka jiwe la msingi shule ya amali Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru wazindua jengo la EMD Peramiho

    May 10, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.