Walimu 1,000 wa shule za msingi na sekondari mkoani Ruvuma wamejitokeza kuwasilisha kero zao wa wajumbe wa Kliniki Maalum ya kushughulikia kero za walimu (Samia Teachers Clinic) kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Walimu hao wamejitokeza kwenye ukumbi wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma mjini Songea katika Timu ya Samia Teachers Clinic ambayo imeanzishwa kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za walimu kote nchini.
Akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kiliwakutanisha walimu Zaidi ya 1,000 kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma,Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Mary Makondo amewapongeza walimu waliojitokeza kuwasilisha kero zao.
“Walimu wengi wamefikiwa na maafisa waandamizi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI wakiwa na laptop kwa ajili ya kutatua kero zao kwenye mifumo’’,alisema Makondo.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Mwl. Edith Mpenzile amesema walimu wamekuwa wanakabiliwa na kero mbalimbali hivyo kitendo hicho kinawatia moyo walimu na kuwa na ari katika uwajibikaji wanapokuwa darasani.
Naye Makamu wa Rais wa CWT Taifa Mwl. Suleiman Ikomba amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili walimu nchini kuwa ni miundo ya utumishi wa walimu,madaraja ya mseleleko,kucheleweshwa kupandishwa madaraja na madai ya mapunjo mbalimbali ya mishahara.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.