Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mwalimu Ephraim Simbeye, amesema kuwa ili sekta ya elimu ipate matokeo yenye ufanisi, ni lazima walimu washiriki mafunzo mbalimbali ili kubadilisha mbinu za ufundishaji.
Amesema hayo wakati akikagua mafunzo ya walimu wa Sayansi na Hisabati yanayoendelea mkoani Ruvuma katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Songea (Songea Girls) manispaa ya Songea.
Mwalimu Simbeye amewaasa washiriki kutumia maarifa wanayopata kuwasaidia walimu wengine ambao hawajapata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo ili yalete tija na matokeo chanya kwa wanafunzi.
Amesisitiza umuhimu wa mafunzo hayo kwa walimu ambapo yatawasaidia kuboresha mbinu za ufundishaji darasani na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanajifunza kwa ufanisi na kuendana na mabadiliko ya wakati.
Ameongeza kuwa sera na mtaala wa elimu wa sasa unawataka walimu kujifunza ili kuendana na mabadiliko chanya na kuhakikisha elimu ya Tanzania inaenda mbele.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.