Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Ngollo Ng’waniduhu Malenya amesema walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalumu wanathawabu kubwa kwa mungu kwa kuwafundisha watoto wenye mahitaji maalumu kwa weledi mkubwa.
‘’Kazi hii ya walimu ni yakitume , nawashukuru walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Namtumbo mnathawabu kubwa kwa mungu “ alisema mkuu wa wilaya ya Namtumbo
Malenya aliyazungumza hayo wakati wa kukabidhi vifaa vilivyonunuliwa kwa michango ya wanawake wa wilaya ya Namtumbo ili kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu waliopo katika shule ya msingi Namtumbo kama sehemu ya mchango wa wanawake wa wilaya ya Namtumbo katika kuathibisha siku ya wanawake duniani.
Mwenyekiti wa kamati ya maadhimisho ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha walimu wilaya ya Namtumbo Anna Mbawala alimwambia mkuu wa wilaya huyo kuwa wanawake wa wilaya ya Namtumbo wamenunua vifaa kwa ajili ya kuwapatia watoto wenye mahitaji maalumu waliopo katika shule ya msingi Namtumbo.
Mbawala alidai vifaa vilivyonunuliwa ni sare za shule ,cherehani,sabuni na vifaa vidogovidogo kama penseli,peni ili kuwarahisishia wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu kupata elimu inayostahili wakiwa shuleni hapo.
Mkuu wa kitengo cha elimu maalumu katika shule ya msingi Namtumbo Bibiana Adamu pamoja na kuwashukuru wanawake wa wilaya ya Namtumbo alisema kitengo katika shule ya msingi Namtumbo kilianzishwa mwaka 1993 kikiwa na mwalimu mmoja na wanafunzi 5 ikiwa wasichana 2 na wavulana 3.
Bibiana alidai kwa sasa kitengo katika shule ya msingi Namtumbo kina jumla ya walimu 4 wanaume 2 na wanawake 2 huku idadi ya wanafunzi ikiwa 49 ,viziwi 9,asiyeona 1,usonji 3, viungo/akili 2 na ulemavu akili 34.
Hata Hivyo Bibiana Adamu alitaja changamoto ya utoro wa wanafunzi unaosababishwa na wanafunzi kukaa mbali,changamoto ya umaskini wa familia wanakotoka watoto hao pamoja na jamii kutokubaliana na hali ya ulemavu ya watoto wao na kuwaficha majumbani
Maadhimisho ya siku ya wanawake wilayani Namtumbo yameathimishwa leo tarehe 7mwezi huu kwa kutoa misaada ya vifaa katika shule yenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu na kutembelea hospitali ya wilaya Namtumbo kuwaona wagonjwa.
Kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ni machi 8kila mwaka na Kauli Mbiu ya siku ya wanawake duniani kwa mwaka huu 2023 ni “Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia ;chachu katika kuleta usawa wa kijinsia”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.