Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, limetekelezwa kwa mafanikio baada ya walimu watano kuhamishiwa Shule ya Msingi Lumalu, iliyoko Kata ya Upolo, wilayani Nyasa. Hatua hii imechukuliwa kufuatia ajali ya gari iliyotokea tarehe 28 Desemba 2024 katika eneo la Burma, wilayani Mbinga, ambapo walimu wanne wa shule hiyo walipoteza maisha.
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Mwalimu Benjamin Kusaga, amewaongoza walimu hao wapya hadi shuleni Lumalu, ambayo ina jumla ya wanafunzi 424 wanaosoma kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.
Pichani, Mwl. Kusaga (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na walimu hao watano waliopangiwa kazini, hatua inayolenga kurejesha hali ya kawaida ya masomo shuleni hapo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.