Na Gustaph Swai -Rs Ruvuma
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi, Dkt. Pindi Chana amewataka wawekezaji waliopewa maeneo katika maeneo ya uhifadhi kuwekeza na kuyaendeleza vinginevyo taratibu za kisheria zitachukuliwa.
Ameyasema hayo alipotembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimkakati katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere Mkoani Ruvuma.
"Kuna watu wameshikilia maeneo katika maeneo yetu ya Uhifadhi, hakuna mtu anaendeleza, hapo unakosesha ajira kwa vijana, Mapato kwa Serikali, hilo hatutaruhusu, Wale waliopewa maeneo katika hifadhi wawekeze lasivyo taratibu za kisheria zitachukuliwa", Alisema.
Akiwa katika ziara hiyo, Balozi Chana amekagua lango la Kitalii la kisasa lakuingilia hifadhini hapo, Mradi wa ujenzi wa kiwanja cha Ndege, Nyumba ya wageni na Ujenzi wa Nyumba za watumishi.
Sanjari na hayo, amebainisha kuwa Nchi ya Tanzania ina vivutio vingi vya Utalii na maeneo ya Wanyama ambapo shughuli mbalimbali za Utalii kama vile Utalii wa uwindaji, upigaji picha na Utalii wa maji.
Ameeleza kuwa Wizara na Jeshi la Uhifadhi limejipanga kuhakikisha rasilimali za Nchi zinalindwa na ametoa rai kwa Wananchi kufuata sheria, kuacha kuchoma moto na kuingiza Mifugo katika Hifadhi.
Kwa Upande wake Kamishna Msaidizi Uhifadhi, Hifadhi ya Taifa ya Nyerere Ephraim Mwangomo amesema ujenzi wa Miundombinu ya hifadhi hiyo ikiwemo lango la kisasa, uwanja wa ndege na Nyumba za watumishi umegharimu Tsh. Bilioni 2.1.
Amewaomba wawekezaji kuja kuwekeza katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere akieleza kuwepo kwa idadi kubwa ya watalii wanaotoa fursa kwa wawekezaji hususani katika eneo la ujenzi wa Nyumba za wageni.
Sekta ya Maliasili na Utalii inachangia pato la Taifa kwa asilimia 17.5 na fedha za kigeni kwa asilimia 25
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.