Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Ruvuma Nicodemus Mwakilembe amewataka walipakodi wote kuwa na utaratibu wakulipa kodi kwa hiari na kwawakati kwani kulipa kodi sio dhambi bali ni uzalendo, ili kuepuka adhabu inayotozwa kwani inaweza ikawa kubwa kuliko kodi anayotakiwa kulipa.
Amesema kulipa kodi ni wajibu wa kisheria hivyo ni jukumu la mlipakodi kutekeleza wajibu huu kwa hiari wa kulipa kodi pamoja na kuwasilisha mawasilisho ya marejesho ya kodi /tax return, huku akiwakumbusha wauzaji nawanunuzi kutoa nakudai risiti katika kila bidhaa.
Kupitia kilele cha wiki ya huduma kwa wateja Mwakilembe amelitaja , lengo la ki hitimisha maadhimisho hayo na wateja wao ofisini hapo ni kuonesha namna ambavyo Wanawajali wateja kwa kuonesha utayari wa kuwahudumia na kujenga ushirikiano baina yao na wateja wao
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.