Halimashauri ya mji wa mbinga mkoani Ruvuma, ni miongoni mwa alimashauri ambazo zinatekeleza na kusimamia mfuko wa afya ya jamii CHF ambapo mpaka sasa mfuko huo tayari umesajili takribani zaidi ya wanachama 14,658 wakiwemo wanufaika wa taasisi mbalimbli kama TASAF,PAD, na Shule za msingi na Sekondari pamoja na Vyuo.
Ndgu; Joseph P. Mapunda ndio mratibu wa utekelezaji wa mfuko huo, anaeleza mwenendo wa utekelezaji wa mfuko huo katika almashauri hiyo.``Tarehe 16/04/2018 tulipokea walaka wa maboresho ya mfuko wa afya ya jamii ikiwa na lengo la kuleta tija na ufanisi katika uratibu wa utoaji huduma ya mfuko wa afya ya jamii kufikia lengo la kitaifa, la kuakikisha kwamba kila kaya iliopo katika jamii inajiunga nakuwa mwanachama hai wa CHF iliyoboreshwa.”
Zaidi ameongeza, Halmashauri ya mji wa mbinga kupitia vikao rasmi kama CMT, CHMT, vikao vya kamati na Baraza la madiwani ,WDC na VDC lakini pia kupitia mikutano mbalimbali ya vijiji na mitaa, CHF limekuwa ni agenda ya kudumu kupitia vikao hivyo vyote.
Uboreshwaji huo umefanywa kwanamna yakipekee ambapo awali mwanachana alikuwa anapata matibabu kwa gharamaya shilingi 10,000.Gharama hizo zilikuwa hazihusishi kulazwa kwa mgonjwa na shilling 20,000 nimalipo yasiona masharti ya kulazwa ispokua utatibiwa katka kituo husika cha afya. Kwa sasa utaratibu umeboreshwa, na kwa kiasi cha shilingi 30,000 unapata matibabu katika hospitali na kituo chochote cha afya katika mkoa wa Ruvuma.
Mwanachama wa bima ya CHF anatakiwa kua na wategemezi wasiozidi 5, hii inafaya jumla ya wanufaika kuwa watu sita kama ni kikundi au taasisi inayo jiunga na mfuko huo, kama ni familia ambayo ukamilisha kaya moja, Baba, Mama na watoto wanne .
Halmashauri ya mji wa mbinga ina kata kumi na tisa(19) Vijiji 49 na mitaa 29 na utekelezaji wa shughuli hii unafanyika katika maeneo yote . Vilevile halmashauri ya mji wa mbinga imefanikiwa kusajili kaya 2448 kati ya kaya 33,256 ikiwa nisawa na asilimia 8.7 ya kaya zote. Pia imefanikiwa, kuwajengea uwezo maafisa uandikishaji 156 katika vijiji na mitaa 78 pamoja na waganga wa vituo23.
Halmashauri ya mbinga mji kupitia mratibu wa TASAF imeweza kusajili kaya 1689 na kuendelea kushirikiana nae katika kuhamsisha jamii hususani kaya masikin kuweza kujiunga katika mfuko huo ili kuweza kuzisaidia kaya hizo kupata huduma ya afya kwa gharama nafuu. Pia tasisi kama PAD kupitia mratibu wao wameweza kusajili kaya 690 usajili bado unaendelea.
CHF Katika halmashauri ya mji wa mbinga pia imejipambanua kuzifikia baadhi ya taasisi za elimu zikiwemo shule za sekondari kama , Makita Sekondari,Agustivo high School, na Chuo cha Maendeleo Mbinga . Atahivyo Mratibu wa CHF Joseph Mapunda Ametoa rai kwa tendaji wa kata ,vijiji na mitaa kuendelea kuwahamasisha wananchi kujiunga katika bima hiyo ya afya ya gharama nafuu, kwani ni mkombozi kwa familia na jamii na kusema zoezi linaendelea watu wajitokeze kwa wingi .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.