WANAFUNZI 54,702 kutoka Halmashauri zote nane mkoani Ruvuma wameanza mtihani wa Taifa wa upimaji katika darasa nne ambao unafanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 25 hadi 26 mwaka huu.
Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Edith Mpinzile amesema kati ya wanafunzi hao Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Ina wanafunzi 9,991,Mbinga Mji wanafunzi 5,222 na Halmashauri ya wilaya ya Nyasa wanafunzi 5,161.
Kwa mujibu wa Afisa Elimu huyo,Halmashauri ya Wilaya ya Songea wanafunzi 5,624,Songea Manispaa wanafunzi 8,508,Namtumbo wanafunzi 8,289,Madaba wanafunzi 1,613 na Tunduru wanafunzi 10,294.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban anawatakia wanafunzi wote wa darasa la nne mkoani Ruvuma,mtihani mwema wa Taifa wa upimaji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.