Wanafunzi wa darasa la awali hadi darasa la nne katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wanatarajia kuanza kupimwa viwango vyao vya uoni na usikivu kuanzia Mei 13 hadi 19, 2024.
Akizungumza katika kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Afisa Elimu Msingi Saada Chwaya amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI imepanga kufanya zoezi hilo litafanyika katika Mikoa minne ambayo ni Ruvuma, Mtwara,Mbeya na Iringa ili kubaini wanafunzi wenye changamoto ya kuona na kusikia.
Kwa upande wake mratibu wa Jifunze uelewe Mkoa wa Ruvuma amesema wanafunzi watakaogundulika kuwa na changamoto za uoni na usikivu watachunguzwa zaidi kitaalam na kupatiwa afua stahiki vikiwemo visaidizi kama vile miwani na shimesikio.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.