Wataalam Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wametoa elimu kwa wanafunzi wa Shule za Msingi kwenye uzinduzi wa wiki ya msaada wa kisheria.
Akitoa Elimu kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Madaba,Mkwera na Njegea Polisi Mkaguzi Msaidizi Antoni Mtokambali amewaeleza wanafunzi kuepuka mazingira ambayo watoto wanafanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Amesema Mazingira hayo ni pamoja na maeneo ya Michezo (PS),mazingira ya usiku,kutorokea porini pamoja na Barabarani.
Hata hivyo amewaeleza Madhara ya ukatili kwa watoto ikiwa suala hilo kusababisha kutoendelea na masomo,kuumizwa kijinsia,Mimba za utotoni,magonjwa pamoja na kifo.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Madaba Shani Kambuga ameelezea haki ya mtoto katika jamii ikiwa mtoto anahaki ya kulindwa,kupatiwa malezi bora,kuishi,kupumzika,haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa,kutobaguliwa, kupewa Jina na Utaifa,huduma bora,kushiriki michezo na shughuli za Nyumbani,haki ya kutoa maoni pamoja na kulindwa.
Kambuga amesema wajibu wa mtoto katika jamii pamoja na kufanya kazi kwaajili ya mshikamano wa familia,kuheshimu wazazi,walezi na wakubwa,kutunza na kuimarisha mshikamano wa familia pamoja na kuimarishau utamaduni
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.