Wanafunzi wa Kidato cha tano na kidato cha sita Shule ya Sekondari Ruanda iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wameahidi kufanya vizuri katika mtihani wao wa kuhitimu kidato cha sita na kusisitiza kuwa wote watapata daraja la kwanza.
Ahadi hiyo imetolewa na Kaka Mkuu wa Sekondari ya Ruanda Oswin Saga alipozungumza kwa niaba ya wananafunzi katika kikao kilichofanyika shuleni hapo hivi karibuni
" Tumeona matokeo ya wenzetu wamefanya vizuri nikuahidi kiongozi kuwa tutashirikiana kwa pamoja na walimu tukizingatia nidhamu na masomo sisi ni divisheni I hayo madaraja mengine ni mwiko kwetu" Amebainisha Oswin
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo mwalimu Paschal Kisese ameeleza kuwa matokeo yajayo yataleta faraja zaidi kwa kuwa ufaulu wa shule hiyo unapanda kila siku hivyo Serikali itegemee matokeo mazuri zaidi ya kidato cha sita kwa mwaka 2025 na kuendelea.
Naye Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Felix Danda amewapongeza walimu na wanafunzi kwa matokeo mazuri ya mtihani wa kidato cha sita yaliyotoka hivi karibuni ametoa rai kwao kuongeza juhudi na jitihada kufikia malengo waliyojiwekea.
Matokeo ya shule hiyo Kidato cha sita mwaka 2024 daraja la kwanza walipata wanafunzi 54 na daraja la pili walipata wanafunzi 27
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.