Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mh. Aziza Mangosongo amewahakikishia mazingira rafiki ya kusomea wanafunzi wote 8,439 waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza katika Wilaya ya Mbinga.
Mh. Aziza amesema idadi ya wanafunzi waliofaulu kwa Halmashauri ya Mji wa Mbinga ni 3,189, huku Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wakiwa 5,250.
Aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea shule za Sekondari za Mbinga na Dkt.. Philip I. Mpango iliyopo katika Kata ya Matarawe na na ile ya Msingi ya Matengo iliyopo Kata ya Matarawe.
Alisema Halmashauri ya Mji wa Mbinga kwa mwaka huu imeandaa vyumba 16 vya madarasa na kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, yenyewe imeandaa vyumba vya madarasa 208.
Wilaya ya Mbinga ina jumla ya shule za sekondari za Serikali 59, ambapo kati ya hizo, 21 zipo katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga na 38 Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.