Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Simoni Bulenganija amesema watoto wote 2082 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2021 wataanza masomo Januari 2021.
Bulenganija ametoa taarifa hiyo wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake Lundusi mji Mdogo wa Peramiho.
“Miundombinu ya vyumba vya madarasa,madawati na vyoo vinatosheleza kwa wanafunzi wote waliochaguliwa,” amesema Bulenganija
Ametoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha mara baada ya shule kufunguliwa watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaripoti katika shuleni walizopangiwa kadiri ya maelekezo ya serikali.
Bulenganija amesema miundo mbinu ya kufundishia na kujifunzia inakidhi mahitaji ,hivyo watoto wote waliochaguliwa wataanza kidato cha kwanza pasipo shaka yoyote na kwamba wazazi na walezi wafanye maandalizi ya kuwawezesha watoto kuripoti shuleni na kuanza masomo.
Hata hivyo amesema serikali inaendelea na ujenzi wa miundo mbinu ya mabweni na vyumba vya madarasa katika shule za Sekondari ya Maposeni,Mpitimbi,Namihoro,Matimira Mbinga mhalule na kilagano na kwamba kukamilika kwa ujenzi wa miundo mbinu hiyo kutaongeza ziada ya miundo mbinu katika Halmashauri hiyo.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa sekondari Bumi Kasege amesema katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na kwamba Idara yake imepanga mikakati ya kusimamia na kufanya ufuatiliaji wa elimu mashuleni na kwa kushirikiana na wadau wa elimu.
Kasege amesema kati ya wanafunzi waliochaguliwa wavulana ni 1013,wasichana ni 1069.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.