Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mh. Wakili Julius S. Mtatiro, amefanya kikao kazi na watendaji Kata, waratibu wa Elimu Kata pamoja na Magavana katika maandilizi ya kupokea wanafunzi mwaka wa masomo 2024.
Katika kikao hicho Mh. Wakili Mtatiro aliwapongeza watendaji hao kwa kazi wanayoifanya katika kata zao, ya kuhakikisha suala la Elimu linapewa kipaumbele. Aliwataka waendelee kufanya kazi kwa bidi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaohitimu elimu ya msingi wanapata fursa ya kujiunga na Elimu ya Sekondari.
Mh. Wakili Mtatiro aliagiza kuhakikisha wanakutana na wazazi/walezi wote ambao watoto wao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ndani ya siku tatu
Mtatiro Pia, aliwataka magavana kupeleleka taarifa ya idadi ya wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka huu ifikapo Januari 9,2024
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.