Mhifadhi wa shamba la miti Wino TFS katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma Groly Fotunatus ametoa rai kwa wananchi wa Madaba kujiunga katika vikundi ili waweze kupewa mizinga ya kufugia nyuki.
Mhifadhi huyo ametoa rai hyo katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya ujenzi katika taasisi za kidini na Serikali kwa Mbunge wa Jimbo la Madaba Dkt.Joseph Mhagama.
Hata hivyo Mhifadhi huyo amewatahadharisha wananchi wahakikishe wanaacha kukata miti na kulima kilimo cha mabondeni badala yake wafuge nyuki.
“Undeni vikundi kupitia Halmashauri,pale ofisini kwangu kuna mizinga 30 inasubiri kikundi hivyo yote hya ni jitihada za kutunza mazingira'',alisisitiza.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.