• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANANCHI Mbinga wafurahia kukamilika kwa kituo cha afya

Imewekwa kuanzia tarehe: May 12th, 2023

WAKAZI wa kata ya Myangayanga katika Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma,wanatarajiwa kuondokana na kero ya kutembea zaidi ya kilomita 7 kwenda hadi Mbinga mjini kufuata huduma za matibabu kufuatia serikali kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa kituo cha Afya kitakachogharimu kiasi cha Sh.milioni 225,000,000.

Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Mtendaji wa kata  hiyo Amos Ndomba alipokuwa akitoa taarifa ya ujenzi kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaibu Kaim.

Ndomba alisema,Halmashauri ya mji Mbinga ilipokea fedha hizo kutoka serikali kuu na utekelezaji wa kituo hicho  ulianza rasmi mwezi Oktoba mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika  ifikapo tarehe 30 mwezi huu.

Alisema, fedha za awamu ya kwanza zimetumika kujenga jengo la maabara na jengo la wagonjwa wa nje(OPD) na majengo hayo yanajengwa kwa mfumo wa force akaunti.

Kwa mujibu wa Ndomba, hadi sasa mradi huo umefikia hatua ya kufunga milango na madirisha na  fedha zilizotumika ni kiasi cha Sh.milioni 218,601,899.00 na kubakiwa na Sh.milioni 40,978,101.00 ambazo zitatumika kukamilisha kazi zilizobaki.

Alisema,wananchi wameshiriki katika ujenzi wa kituo hicho kwa kuchana mbao 2248 zenye thamani ya Sh.milioni 8,660,500,kusafisha eneo Sh,milioni 100,000,kuchimba msingi Sh.100,000,kulipa fidia ya eneo Sh.500,000 na wadau wengine wamechangia fedha taslimu kiasi cha Sh.220,000.

Aidha alisema,mradi huo ulikabiliwa na changamoto mbalimbali wakati wa utekelezaji  ikiwemo uhaba wa maji kipindi cha kiangazi na kusababisha ujenzi kusimama mara kwa mara hadi maji yalipopatikana na mvua kubwa iliyonyesha mwezi Disemba ilisababisha wananchi kushindwa kusomba mbao kutoka msituni.

Alisema,ujenzi wa kituo cha afya Myangayanga ukikamilika utasaidia sana kupungua kwa rufaa za wagonjwa kutoka zahanati za jirani kwenda Hospitali ya Halmashauri ya Mji,kupunguza adha  kwa wananchi ya kufuata huduma za afya umbali mrefu.

Alitaja faida nyingine za mradi huo  ni pamoja na kuongezeka kwa huduma za kiuchunguzi kupitia maabara,kuwepo kwa huduma za upasuaji kwa akina  mama wajawazito na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa akina mama na watoto.

Mwenyekiti wa kijiji cha Myangayanga Aidan Mwingira,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa kutoa fedha za kujenga kituo cha afya Myangayanga na viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa kwa ushauri na usimamizi wao.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka 2023 Abdalla Shaibu Kaim,amempongeza  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mbinga Grace Quintine, kwa kazi nzuri ya kuibua na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kusogeza na kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi wa Mbinga.

Kiongozi huyo  wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2023,ametoa wiki mbili kwa Halmashauri ya mji Mbinga kukamilisha ujenzi wa kituo hicho ili wananchi waanze kupata huduma za matibabu.



Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.